Dirisha dogo limesogezwa mbele, Elias Maguri anaelekea Wapi? afunguka haya

Dirisha dogo limesogezwa mbele, Elias Maguri anaelekea Wapi? afunguka haya

0
SHARE

Dirisha dogo limesogezwa mbele,Elias  Maguri anaelekea Wapi? afunguka haya

Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars ” Elias Maguri ambaye kwasasa ni mchezaji huru amefunguka kuhusu hatma yake wakati huu.

Wengi wanahoji kuwa baada ya dirisha dogo kusogezwa mbele je Elias Maguri ataelekea wapi? Mara baada ya kuwa akihusishwa na baadhi ya Vilabu ikiwemo Yanga ya jijini Dar Es Salaam.

Maguri msomaji wa Kwataunit amesema kuwa Hafikirii kucheza Tanzania kwasasa na tayari ameshaenda nchini Afrika Kusini kumalizana na timu ya Polokwane inayoshiriki ligi kuu nchini Afrika Kusini PSL

” Ni kweli nilienda Afrika Kusini mara baada ya mchezo dhidi ya Zanzibar (CECAFA) nikakutana na viongozi wao na tukamaliza baadhi ya mambo na nikasaini mkataba wa awali”

Maguri ambaye alianza kuwavutia Polokwane na baadhi ya vilabu nchini humo wakati wa kombe La COSAFA mwaka huu amesema Watanzania wasubiri mambo yakikamilika ataweka wazi kila kitu.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY