Je Simba wamemalizana na Lipuli kwa Asante Kwasi? Majibu haya hapa

Je Simba wamemalizana na Lipuli kwa Asante Kwasi? Majibu haya hapa

0
SHARE
Asante Kwasi Simba
Asante Kwasi Simba

Je Simba wamemalizana na Lipuli kwa Asante Kwasi? Majibu haya hapa

Baada ya kuwepo taarifa kwenye mitandao ya kijamii kuwa Simba wameshamalizana na Lipuli kuhusu mchezaji  Asante Kwasi  Klabu ya Lipuli imeibuka na Kupinga taarifa hizo.

Mwenyekiti wa Klabu ya Lipuli Ramadhan Mahano amesema kuwa hawajapokea Ombi lolote wala hawajafanya mazungumzo yoyote na Klabu ya Simba kuhusiana na Suala la Usajili wa Asante KWASI.

“Taarifa ambazo ziko kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na Sisi kumalizana na Simba siyo za Kweli sisi hatkafanya mazungumzo yoyote na Simba kuhusiana na usajili wa Asante Kwasi kama ambavyo mitandao inasema “

Aidha msomaji wa Kwataunit.com Mahano amesema kutokana na Asante Kwasi kutoripoti kambini kama ambavyo walivyokubaliana awali wamemwandikia barua ya kumjulisha kuripoti kituo chake cha kazi mapema kabla ya hatua za Kinidhamu kuchukuliwa juu yake.

>> Mzee Akilimali, Simpingi Manji<<

Taarifa za Simba kumalizana na Asante Kwasi zimekuja siku kadhaa mara baada ya TFF kusema wameongeza dirisha mpaka december 23, 2017 kutokana na mtandao wa FIFA kuwa na matatizo ya kuwasilisha majina hayo.

Lakini Taarifa ambazo TFF wamezitoa  msomaji wa Kwataunit kutoka kwa afisa habari wake Alfred Lucas wamesema kuwa tayari mtandao huo umekaa sawa na sasa Vilabu vinaweza kumalizia kazi iliyokuwa imebakia.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY