Laudit Mavugo ataja timu 2 zilizofanya naye mazungumzo

Laudit Mavugo ataja timu 2 zilizofanya naye mazungumzo

0
SHARE

Laudit Mavugo ataja timu zilizofanya naye mazungumzo

Mshambuliaji wa timu ya Simba Laudit Mavugo amekiri kufanya mazungumzo na klabu mbili za Nchini Kenya baada ya kuwepo taarifa za kutemwa ndani ya Kikosi cha Simba wakati huu wa dirisha dogo.

Mavugo ambaye ni Raia wa Burundi amekiri kufanya mazungumzo na timu mbili vigogo nchini Kenya AFC Leopards na Gor Mahia ambao ni kama Simba na Yanga za nchini Kenya.

Mavugo aliyejiunga na Simba msimu uliopita akitokea nchini Burundi katika klabu ya Vital’O  msomaji wa Kwataunit amesema yeye anapenda kama Simba watamuacha basi acheze nchini Kenya na siyo Oman kama ambavyo imekuwa ikidaiwa huenda Mavugo akapelekwa kwa Mkopo.

>> Said Mohammed Nduda siku zinahesabika Simba <<

Simba tayari inadaiwa kuleta washambuliaji wawili Domingos na Sakuwaha kwaajili ya kumimarisha idara ya Ushambuliaji hali inayotajwa kuwa huenda ikawa ni ishara ya kumwambia Mavugo bye bye Simba.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY