Haji Manara anavyotamani Okwi,Bocco kuwa Ronaldo au Messi Leo

Haji Manara anavyotamani Okwi,Bocco kuwa Ronaldo au Messi Leo

0
SHARE

Haji Manara anavyotamani Okwi,Bocco kuwa Ronaldo au Messi Leo

Ni wazi kuwa moja kati ya siku kubwa katika soka la Tanzania ni leo kwani kutakuwa na moja kati ya mechi Ngumu katika Ligi kuu Tanzania Bara mechi kati ya Simba na Singida United uwanja wa Taifa jijini Dar Es Salaam.

Kwanini Manara anatamani Okwi awe kama Ronaldo au Messi kwa Leo na Siyo Siku nyingine.

Hakika leo ni siku ya Furaha kwa Haji Manara kwani anasherehekea siku yake ya Kuzaliwa na ni wazi kuwa atakuwa na Furaha na kwa jinsi ambavyo Manara ni shabiki kindakindaki wa Simba na siyo tu kiongozi ndani ya Simba kwani ni wazi Manara anaipenda sana Simba, Kufungwa kwa Simba kutamfanya Manara na siku yake ya kuzaliwa kuwa Mbaya sana.

Ni wazi dunia ya sasa katika soka inawaongelea wafalme wawili Ronaldo na Messi na ndivyo kichwani Haji Manara anawaza na Kutamani leo Okwi  au Bocco wavae viatu vya wachezaji hao wawili ili kuipa Simba Ushindi, Kuipa Simba points 3 na Kumpa Haji Manara Furaha katika Siku ya leo.

Naamini Manara leo msomaji wa Kwataunit.com ataongea na wachezaji wa Simba hasa washambuliaji wa timu hiyo kama John Bocco Mosses Kitandu na Emmanuel Okwi kuwaomba chonde chonde kutomwangusha katika siku yake ya Leo.

Kukosa Ushindi kwa Simba leo dhidi ya Mwadui Haji Manara ni wazi atapata shida mitandaoni kwani amekuwa na kawaida ya kuwa na utani kwenye mitandao hasa mtandao wa Instagram.

UGUMU WA MCHEZO UKO WAPi?

Ni wazi kuwa mechi itakuwa ngumu hasa kutokana na ubora wa vikosi vya Timu zote mbili, uzito wa vikosi vya timu zote, wachezaji wenye uzoefu, Makocha wenye uzoefu mkubwa na Upinzani uliopo katika msimamo ni vitu ambavyo vinaenda kunogesha mchezo wa leo.

Singida upande wa benchi la Ufundi wanaweza wakawa na faida zaidi kwani Mwalimu HANS Van Pluijm anaijua vyema Simba na Soka la Tanzania Kuliko mwalimu Masoud Djuma

Simba nao wanajivunia kuwa na Kikosi Kipana huku kurejea kwa baadhi ya Nyota wake Muhimu kukiwafanya Kujiamini zaidi kuelekea Mchezo wa Leo. Yote kwa Yote tusubiri dakika tisini za Mchezo wa Leo Kumbuka Kwataunit.com tutakupa Kila Taarifa kuanzia vikosi mpaka matokeo ya moja kwa Moja.

 

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY