Achana na Hat trick za Chirwa na Okwi Huyu ndiye Mbabe wa...

Achana na Hat trick za Chirwa na Okwi Huyu ndiye Mbabe wa Hatrick Tanzania

0
SHARE
Yanga na St Louis mara ya Mwisho Kukutana mambo yalikuwa Hivi

Achana na Hat trick za Chirwa na Okwi Huyu ndiye Mbabe wa Hatrick Tanzania

Ukiachana Na Hat-rick (Kufunga goli 3 katika mchezo mmoja)  za Obrey Chirwa wa Yanga ambaye amekuwa Gumzo kutokana na Kutupia kwake Hat Trick Yake ya Pili msimu Huu, Huku Emmanuel Okwi akiwa na Hat Trick Moja pekee lakini Ndani ya kipindi cha Miaka 5 yupo Mbabe wao.

Katika Kipindi cha Miaka 5 Iliyopita  msomaji wa Kwataunit Amis Josylin Tambwe ndiye mbabe wa Hat Trick Tanzania Kutokana na Kuwa nazo nyingi zaidi, Tambwe anajumla ya Hat Trick 5 ndani ya Kipindi hiki akiwa alifunga mbili akiwa Simba na 3 akiwa Yanga.

Akiwa Simba msimu wa Mwaka 2013/2014 Tambwe alifunga Hat Trick 2 moja Simba dhidi ya Mgambo JKT ambapo Simba ilishinda bao 6 kwa 0, Tambwe akitupia 4 peke yake.

Huku Nyingine akiwa Simba alifunga dhidi ya Oljoro JKT msimu huo huo wa 2013/2014 Simba ikishinda 4 kwa 0.

Baada ya Hapo alihamia Yanga na Katika msimu wa 2014/2015 Tambwe alifanikiwa kufunga Hat Trick Yake ya Kwanza Yanga ikicheza dhidi ya Coasta Union na Kushinda bao 8 kwa 0 Tambwe akifunga bao 5 peke yake, Hapo Coastal ilikuwa chini ya Julio.

Msimu wa 2015/2016 Tambwe alifanikiwa Kufunga Hat Trick Mbili Moja Dhidi ya Maji Maji na Nyingine dhidi ya Stand United.

Katika msimu Uliopita Kuna Hat trick Mbili pekee ndizo zilitokea VPL ambapo moja Ilitoka kwa Kelvin Sabato “Kiduku” akichezea Stand United wakati Stand Ikiiua Mtibwa Sugar Na Nyingine ikiwa ni ya Abdulrahman Mussa wa Ruvu Shooting.

Chirwa Kafikia Rekodi ya Tambwe ndani ya Msimu mmoja,Hat Trick 2.

Obrey Chirwa msomaji wa Kwataunit.com  amefikia Rekodi ndani ya Misimu Hii Mitano ya Kufanikiwa kufunga zaidi ya Hat Trick Moja kwenye msimu mmoja, Ndani ya Misimu yote Hii mitano hakuna Mchezaji hata Mmoja Ukiachana na Tambwe ambaye aliwahi kufanya Hivyo lakini Chirwa amefikia Rekodi Hiyo.

Anadaiwa 3.

Ili afike kwenye Rekodi ya Tambwe inambidi Chirwa afunge Hat Trick nyingine 3.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY