Habari Mpya Simba leo February 13, 2018

Habari Mpya Simba leo February 13, 2018

0
SHARE

Habari Mpya Simba leo February 13, 2018

Klabu ya Simba inatarajia Kuondoka leo kuelekea Mkoani Shinyanga kuwakabili Mwadui Fc huku wakienda kwa tahadhari kubwa kutokana na kiwango kizuri ambacho kimeonyeshwa na Mwadui katika mchezo uliopita.

Afisa Habari wa Klabu ya Simba Haji Manara ameithibitishia Kwataunit.com kuwa wao kama Simba hawaichukulii timu yoyote Poa na Wanajua Fika kuwa Ubingwa bado kutokana na Timu yoyote ile katika Ligi inaweza kuwa kufikisha Points ilizonazo Simba wakati ili uwe Bingwa inabidi uwe na Points ambazo timu nyingine haziwezi kufikia.

 

” Mwadui ni Timu nzuri umeona mechi ya Mwisho wamemfunga Mtibwa bao tatu kwahiyo hatuwezi kuwadharau ” 

 

Katika Mchezo kati ya Mwadui ya Mjini Shinyanga na Simba mchezo utakaochezwa mjini Shinyanga katika uwanja wa ccm Kambarage Simba itamkosa mlinzi wake wa Kushoto ambaye amekuwa mwiba pia kwenye Ufungaji msimu Huu Asante Kwasi.

Kwasi atakosekana kutokana na Kuwa na Kadi 3 za Njano hali inayomfanya kukosa Sifa ya Kucheza mchezo unaofuata.

Akiongea Kuhusu Al Masri  msomaji wa Kwataunit.com MANARA amesema kama Simba watafuzu na Al Masry watafuzu basi Maandalizi yatakuwa makubwa zaidi kutokana na Ubora wa Timu hiyo.

” Always wamisri wanakuwa vizuri na wanatimu nzuri kuliko Tanzania  Kama Al Masry watafuzu basi tutafanya maandalizi makubwa zaidi kuliko haya tuliyokuwa nayo lakini kwasasa tunaelekeza maandalizi kwenye mchezo wa marudiano na Wadjibout “

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY