Maradona agoma kuingia Marekani baada ya Kumuita jina Hili Baya Trump

Maradona agoma kuingia Marekani baada ya Kumuita jina Hili Baya Trump

0
SHARE

Mkongwe wa Soka duniani Diego MARADONA raia wa Argentina mwenye miaka 57 kwasasa  amegoma katakata kwenda nchini Marekani baada ya kumtusi Rais wa sasa wa Marekani Bw. Donald Trump akifanyiwa Mahojiano kwenye kituo cha TV.

Maradona amesema amegoma kuchukua Visa ya kuingia Marekani  mara baada ya Kumtusi rais wa Taifa Hilo Donald Trump.

Mchezaji huyo wa zamani ambaye kwasasa ni manager wa timu ya Al Fujairah huko Uarabuni alikuwa akifanyiwa mahojiano  kupitia kipindi kimoja maarufu kwa jina la ” Buenos dias America ” na ndipo alipolitibua.

Maradona anatakiwa kwenda Marekani kwaajili ya Kesi na Mpenzi wake wa zamani Claudia Villafane.

Hata hivyo Star huyo  msomaji wa Kwataunit amewahi kuondolewa Marekani mara baada kukutwa na madawa ya Kulevya wakati wa kombe la dunia mwaka 1994.

WAKILI WAKE ASIMULIA KILA KITU

Wakili wake Matias Morla amesema wakati Mteja wake Maradona anakwenda kwenye kipindi alimsisitizia asiongee ubaya wowote kuhusu Marekani kwani yeye alikuwa ubalozini kufatilia Viza.

Lakini chaajabu swali la Pili tu kuulizwa Maradona povu likamtoka, Kwani Aliulizwa Unafikiria nini Kuhusu Donald Trump?

Maradona Akajibu

” Trump kwangu ni  Chirolita (hili Ni neno linalotumika kumaanisha kitu kama  sanamu ya mtu au katuni ya mtu )

Baada ya Kauli hiyo wakili wake ilibidi aamue jukumu la yeye kwenda Marekani kumwakilisha.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY