Masoud Djuma : Wachezaji hawa Simba wanahitaji mtaalamu wa Saikolojia

Masoud Djuma : Wachezaji hawa Simba wanahitaji mtaalamu wa Saikolojia

0
SHARE
masoud djuma Simba
masoud djuma Simba

Masoud Djuma : Wachezaji hawa wanahitaji mtaalamu wa Saikolojia

Kocha msaidizi wa Timu ya Simba Mburundi Masoud Djuma amesema kuwa wachezaji ambao wanakosa nafasi katika kikosi cha Simba wanahitaji mtaalamu wa Saikolojia.

Masoud msomaji wa Kwataunit.comĀ  Amesema kikawaida kwa mchezaji anayejitambua anapokosa nafasi ya kucheza kikosi cha Kwanza huwa anaongeza juhudi katika mazoezi ili apate nafasi lakini kwa Simba ni Tofauti.

Kocha huyo mtaalamu wa Mfumo wa 3-5-2 amesema Kwa Simba imekuwa tofauti kwani wale wanaopata nafasi kikosi cha Kwanza ndiyo wamekuwa wakijituma zaidi mazoezini kuliko ambao hawapati nafasi.

Kwa Hali hiyo Masoud anatamani wachezaji hao labda wapate mtaalamu wa Saikolojia ili kuweza kuwaweka sawa wachezaji ambao wamekuwa hawapati nafasi ya Kuanza au kucheza katika kikosi cha Simba kiasi cha Kuonekana wachezaji walewale katika mechi Nyingi.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY