Matokeo UEFA champions League 14 February 2018

Matokeo UEFA champions League 14 February 2018

0
SHARE

Matokeo UEFA champions League 14 February 2018

Timbwili Timbwili la UEFA champions league hatua ya 16 bora inaendelea na katika michezo ya Jana kulikuwa na Mechi mbili mchezo kati ya FC Porto na Liverpool na Mchezo mwingine ukiwa kati ya Real Madrid na PSG.

Fc Porto vs Liverpool 14.2.2018

Mechi kati ya Fc Porto na Liverpool mechi hiyo Iliisha kwa Liverpool kushusha Kipigo cha hatari licha ya Kuwa Ugenini kwa kuwafunga Porto kwa bao 5 kwa 0.

Magoli ya Liverpool yakifungwa na Sadio Mane aliyefunga jumla ya Mabao 3, Huku Mabao mengine mawili yakifungwa na  Mohammed Salah na Roberto Firmino.

Real Madrid vs PSG 14.2.2018

Katika mchezo uliokuwa ukisubiriwa kwa Hamu msomaji wa Kwataunit.com  hakika ni Huu lakini Madrid wakamaliza kwa kuibuka kwa Ushindi mkubwa wa bao 3 kwa 1.

Christiano Ronaldo akaibuka mbabe kwa kufunga mabao mawili na Goli moja la tatu likifungwa na Marcelo dakika ya 86, Bao la PSG lilifungwa na Adrien Rabiot dakika ya 33.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY