Simba kikombe Hakiepukiki kwa Mwarabu,Yanga wapata Unafuu baada ya Hili

Simba kikombe Hakiepukiki kwa Mwarabu,Yanga wapata Unafuu baada ya Hili

0
SHARE

Simba kikombe Hakiepukiki kwa Mwarabu,Yanga wapata Unafuu baada ya Hili

Wakati Simba wakifurahia ushindi wa Timu yao dhidi ya Gendarmerie ya Djibouti wa Bao 4 kwa 0 na hali ikionekana wazi kuwa Shughui Imeisha kwani katika mechi ya Marudiano WaDjibouti watahitaji kushinda kuanzia Goli 5 kwa 0  hali ambayo Kwa Simba ya sasa na Hao Gendarmerie wenyewe walivyoonekana siyo Rahisi.

Kwahiyo msomaji wa Kwataunit ni wazi kuwa Simba ananafasi kubwa ya Kupita kwenda hatua Inayofuata na Dalili zinaonyesha wazi kuwa huenda Simba wakakutana Na Waarabu kutoka Misri El Masry ambao nao walishinda bao 4 kwa 0 kama Simba katika Mechi yao ya awali.

YANGA WAPATA NAFUU YA KUMUEPUKA MWARABU 

Sasa Yanga huenda akaepuka Kikombe cha Mwarabu Kutoka Sudan Al Merreikh mara baada ya Mabingwa hao wa Sudan kukubali kuchapwa bao 3 kwa 0 katika mchezo wao wa awali dhidi ya Township Rollers ya Botswana.

Kwahiyo Al Merreikh watahitaji kushinda kuanzia bao 4 kwa 0 ili Kuvuka hatua Inayofuata, Hali ambayo huenda isiwe kazi nyepesi sana kwa wao Kufanya Hivyo lakini siku zote Mpira Unadunda na Maamuzi ya Mwisho huwa yanabaki baada ya Dakika 90 uwanjani.

Kupenya kwa Wabotswana  msomaji wa Kwataunit.com kunaweza kusiwaogopeshe sana Yanga ukilinganisha na Waarabu ambao wamekuwa wakiisumbua sana Yanga katika michuano ya Kimataifa mara nyingi wanapokuatana

 

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY