Yanga na Donald Ngoma Kimeeleweka,Ishu kamili imekaa hivi

Yanga na Donald Ngoma Kimeeleweka,Ishu kamili imekaa hivi

0
SHARE
donald-ngoma-yanga

Yanga na Donald Ngoma Kimeeleweka,Ishu kamili imekaa hivi

Siku chache baada ya Uongozi wa Yanga kudaiwa kuwa katika mipango ya Kuvunja Mkataba na Mchezaji Donald Ngoma, Mapya yameibuka kuhusu sakata la Yanga na Mchezaji huyo.

Ngoma, ambaye anaendelea kuuguza majeraha yake ya goti, anategemewa kuanza mazoezi wiki hii baada ya kudaiwa kupona.
Yanga inayodhaminiwa na Kampuni ya Kubashiri Matokeo Michezoni ya SportPesa, kwa sasa inaendelea na mazoezi yake kwenye Uwanja wa Chuo cha Polisi Kurasini ikijiandaa na mchezo ujao wa Ligi Kuu Bara.

Mmoja wa viongozi wa timu Akiongea nasi jana amesema Ngoma anajiandaa kurejea uwanjani hivi karibuni, hivyo suala la kukatishwa mkataba wake limesitishwa.

“Hayo yalikuwa mapendekezo, kwamba kama hatorejea uwanjani kwa muda mrefu ni vyema mkataba wake ukakatishwa, lakini Ngoma ameanza kupona na hivi karibuni ataanza mazoezi mepesi kabla ya kuungana na wenzake,”

alisema kiongozi huyo ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini.
Kwa upande wake, Meneja wa klabu hiyo, Hafidh Saleh, alimwambia mwandishi wetu kuwa taarifa alizonazo juu ya mshambuliaji huyo ni kuwa anaendelea kupona na hivi karibuni atarejea uwanjani.

“Hayo masuala ya mkataba ni ya uongozi zaidi, mimi binafsi sifahamu, ninachojua Ngoma anaendelea kupona na mwenyewe amesema anakaribia kurejea uwanjani,” alisema Saleh.
Alisema amewasiliana na mchezaji huyo na kumhakikishia kuwa taratibu ameanza kupona na anatarajia kuanza mazoezi hivi karibuni.

Wiki iliyopita, Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa, alikaririwa akisema kuwa wanafikiria kuuvunja mkataba na nyota huyo kwa kuwa amekuwa na majeraha ya muda mrefu.

Katika hatua nyingine, Yanga imepanga kuelekea Shelisheli mapema zaidi kwa ajili ya mchezo wao wa marudiano wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya klabu ya St Louis ya nchini humo.

Katika mchezo wa kwanza uliochezwa Jumamosi iliyopita, Yanga ilifanikiwa kupata ushindi wa bao 1-0.
Ili kusonga mbele, wawakilishi hao wa Tanzania Bara wanahitaji ushindi ama sare ya aina yoyote katika mechi hiyo ya marudiano.

source : Nipashe

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY