Yanga na St Louis mara ya Mwisho Kukutana mambo yalikuwa Hivi

Yanga na St Louis mara ya Mwisho Kukutana mambo yalikuwa Hivi

0
SHARE
Yanga na St Louis mara ya Mwisho Kukutana mambo yalikuwa Hivi

Yanga na St Louis mara ya Mwisho Kukutana mambo yalikuwa Hivi

Kama ulifikiri Yanga haijawahi kukutana kabisa na ST. Louis ya Sheli sheli basi utakuwa unajidanganya kwani imewahi kutokea.

Mwaka 1992 Yanga na St. Louis  msomaji wa kwataunit.com zilikutana kwa mara ya mwisho Yanga ikiwakilisha Tanzania katika michuano ya klabu Bingwa wakati huo huo St. Louis nayo ikiiwakilisha Sheli Sheli katika michuano hiyo Inayoandaliwa na Shirikisho la soka barani Afrika CAF.

Wakati huo ilikuwa inajulikana kama St Louis kabla ya kuungana na klabu nyingine ya  Sunshine mwaka 2007 na kujulikana kama St. Louis Suns United (Iliyopo mpaka sasa)

Katika mwaka Huo Yanga iliifanyia Umafia timu ya St. Louis kwani iliichapa bao 7 kwa 2 kwa matokeo ya jumla klabu hiyo.

Yanga ilianza kwa kushinda bao 3 kwa 1 Ugenini nchini Sheli Sheli na Kisha wakawaadhibu bao 4 kwa 1 walipotua nchini Tanzania katika mechi ya Marudiano na kufanya matokeo ya mwisho kuwa 7 kwa 2.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY